Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

Tanoil Investments Limited

KUHUSU SISI

Kwa Ufupi

Tanoil Investments Limited ni Kampuni ya Biashara ya Mafuta (OMC) iliyopo Dar es Salaam, Tanzania; ni Kampuni Tanzu inayomilikiwa kikamilifu na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na ilianzishwa na kusajiliwa kufanya biashara ya mafuta kama inavyoelezwa chini ya Sheria ya Petroli (Sura ya 21, Toleo Lililofanyiwa Marekebisho ya mwaka 2015).

Kampuni ilianzishwa rasmi tarehe 22 Machi 1999 kwa jina la Commercial Petroleum Company (COPEC) ikiwa na cheti cha usajili namba 35975. Jina la COPEC lilibadilishwa kuwa Tanoil Investments Limited tarehe 1 Novemba 2017. Kampuni imepewa leseni na mamlaka husika zikiwemo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), n.k.

Kampuni yetu ilianza shughuli zake za kibiashara mwezi Machi 2021 na kuongeza wigo hatua kwa hatua kwa kutumia uwekezaji wa mtaji kutoka Kampuni mama (Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania).

Kampuni yetu inawakilisha maslahi ya kimkakati ya Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania katika miradi yote ya petroli ya ngazi ya kati (midstream) na ngazi ya chini (downstream). Hii inajumuisha maendeleo ya miundombinu kama vile viwanda vya uchenjuaji wa mafuta, mabomba ya kusafirisha mafuta, pamoja na mifumo ya kitaifa ya ugavi na usambazaji wa bidhaa za petroli.

Shughuli za ‘midstream’ zinahusisha uchenjuaji wa mafuta, uchakataji wa petrochemical, na miundombinu ya usafirishaji zikilenga kuongeza thamani ya bidhaa za petroli na kuimarisha uwezo wa taifa katika sekta ya nishati. Shughuli za ‘downstream’ zinajumuisha biashara ya usambazaji wa bidhaa za petroli kote nchini.

Ofisi yetu makuu ipo katika Jengo la Benjamin William Mkapa, Barabara ya Azikiwe/Jamhuri, Posta, Dar es Salaam, Tanzania. Tumejizatiti kuunga mkono usalama wa nishati wa Tanzania na ukuaji wa uchumi kupitia suluhisho bora, endelevu, na zenye kuongeza thamani katika sekta ya petroli.