Wasifu wa James Shangari Sanawa
Kaimu Meneja Mkuu
James Shangari Sanawa ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tanoil Investments Limited tangu Aprili, 2023. Hapo awali, alishikilia nafasi hiyo kati ya Mei 2017 na Oktoba 2018. Kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Meneja Mkuu, alikuwa Meneja wa Biashara ya Mafuta katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) tangu mwaka 2014.
James Shangari Sanawa ameweza kuleta mabadiliko makubwa katika kampuni kwa kuweza kuimarisha mazingira ya kibiashara yanayohusu taratibu za ndani na wateja wake pamoja na wadau wa biashara ya mafuta. Mazingira hayo ya biashara yameweza kufungua njia katika kuendeleza biashara ya mafuta. Kabla ya kujiunga na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na baadaye Tanoil Investments Limited, alifanya kazi katika Benki ya Posta Tanzania (TPB), ambayo kwa sasa inajulikana kama Benki ya Biashara Tanzania (TCB).
Kampuni yetu hapo awali ilijulikana kama COPEC (ambayo haikufanya kazi kwa miaka 18), James Shangari Sanawa ni Meneja Mkuu mwanzilishi ambaye aliifufua kampuni mnamo Novemba 2017 na ana uzoefu mkubwa katika sekta ndogo ya petroli ikiwa ni pamoja na usimamizi wa miradi, biashara ya mafuta miongoni mwa mengine.
James Shangari Sanawa ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtaalamu wa usimamizi wa biashara kwa mafunzo, alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Coventry, Uingereza na Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara katika Sekta ya Mafuta na Gesi mwaka 2013, kabla ya hapo alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Mysore (India) na Shahada ya Kwanza ya Usimamizi wa Biashara mwaka 2001. Zaidi ya hayo, alisoma Shahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhitimu Shahada ya Sheria. Bwana Sanawa ni mwanachama hai wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), chama cha kitaaluma cha mawakili nchini Tanzania Bara.
Kampuni imerekodi mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa hatua kadhaa za kurahisisha biashara kupitia nyaraka za kazi, sera na taratibu sanifu za uendeshaji; na hivyo kuibadilisha kampuni kutoka kuwa inayopata hasara hadi kuwa kampuni tanzu inayopata faida.
Kampuni hivi sasa inaagiza na kukomboa shehena zake kupitia malipo ya fedha taslimu au barua za mikopo kwa wakati. Kodi na tozo zenye thamani ya makumi ya mabilioni zimelipwa na kuendelea kulipwa, na hivyo kuchangia uchumi. Katika nyakati kadhaa, nchi imekuwa katika hatari ya uhaba wa mafuta, ambapo, Kampuni imekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi haiingii katika usumbufu wa usambazaji wa mafuta.
Kampuni yety ni taasisi tanzu iliyopo chini ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) iliyoingizwa kwenye usajili kwa chet Na35975 mwaka 1999 kama Kampuni ya Uuzaji wa Mafuta. kampuni hii Imesajiliwa na Wakala wa Ununuzi wa Pamoja wa Mafuta (PBPA) kwa leseni ya biashara ya mafuta iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA). Hadi sasa kampuni inaendelea kujivunia na kufurahia huduma ya kuuza mafuta kwa umma (Mashirika na Taasisi za Serikali) na wateja wa sekta binafsi wa jumla na rejareja.