Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

Tanoil Investments Limited

Majukumu

Majukumu ya Kampuni

Kuendesha biashara ya bidhaa za petroli kunakohusisha kushiriki kikamilifu ununuzi, uhifadhi, usafirishaji, masoko, usambazaji na uuzaji wa aina mbalimbali za bidhaa za petroli na zinazohusiana na petroli, ikiwemo vilainishi (lubricants), gesi ya petroli iliyosindikwa (LPG), pamoja na bidhaa nyingine za nishati.

Biashara yetu inajumuisha shughuli za ngazi ya kati (midstream) na ngazi ya chini (downstream) ikiwemo biashara ya jumla na rejareja, uendeshaji wa maghala ya kuhifadhia mafuta, mabomba ya kusafirisha mafuta, vituo vya kuhudumia na kujazia mafuta, pamoja na uanzishaji wa mifumo bora ya ugavi na usambazaji ili kuhudumia wateja wa viwandani, kibiashara na wa rejareja.

Biashara yetu ya bidhaa za petroli pia inahusisha uendelezaji wa ushirikiano wa kimkakati na ubunifu ili kuongeza ufanisi wa uendeshaji, kukabiliana na mabadiliko ya soko, na kutoa suluhisho za nishati zenye uhakika na ubora wa hali ya juu zinazochangia maendeleo ya uchumi, usalama wa nishati, pamoja na mahitaji yanayobadilika ya masoko ya ndani na ya kikanda.