Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

Tanoil Investments Limited

Maadili ya Msingi

Maadili Yetu:

Katika kuendesha shughuli zake za kibiashara, Kampuni yetu inaongozwa na maadili yafuatayo ya msingi

Ubora
Kampuni imejipanga kutoa huduma bora ubora ikizingatia ubunifu na ukuaji endelevu kwa kufanya maamuzi yanayotegemea ushahidi na kuzingatia mtazamo wa kibiashara ili kuanzisha masoko mapya, bidhaa na huduma, na kutoa huduma zenye viwango vinavyokubalika.

Uaminifu na Ushirikiano
Kampuni inakuza utamaduni wa uaminifu, kufanya kazi kwa kushirikiana, heshima, ambapo maadili ya uadilifu, uwazi, uwajibikaji na weledi yanathaminiwa, hivyo kuhakikisha ushirikiano na mawasiliano yenye ufanisi kati ya timu yetu.

Ubunifu
Kampuni yetu ina shauku kubwa ya ubunifu ikichochea maendeleo ya vyanzo vya nishati endelevu, nafuu na bunifu vinavyowezesha maisha ya watu na kujenga mustakabali bora zaidi.

Kumlenga Mteja
Kampuni yetu inawaweka wateja mbele katika kila jambo kwa kusikiliza kwa makini sauti ya mteja, tunajitahidi mara kwa mara kuzidi mahitaji na matarajio yao.