Dhima yetu
Kampuni imedhamiria kutoa bidhaa za petroli zenye ubora wa hali ya juu, kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa bidhaa, bei shindani, usafirishaji na ugavi wenye ufanisi hadi maeneo ya mbali, pamoja na huduma bora kwa wateja, kwa kuzingatia kikamilifu viwango bora vya sekta na matakwa ya kisheria. Kupitia dhamira hizi, Kampuni inalenga kuimarisha nafasi yake kama mtoa suluhisho kinara wa nishati huku ikichangia ukuaji wa uchumi na usalama wa nishati nchini Tanzania na katika soko pana la kikanda.
Bidhaa zinazopatikana sasa;
Dizeli (AGO): Mafuta ya dizeli ya ubora wa juu yanayofaa kwa matumizi ya magari, viwandani na kibiashara.
Petroli (PMS): Usambazaji wa petroli ya kiwango cha juu kwa matumizi ya magari na matumizi ya kawaida.
Soko letu;
Taasisi za Serikali: Tunahudumia kwa ukaribu taasisi za umma katika sekta zote zikiwemo nishati, usafirishaji na ujenzi.
Shughuli za Uchimbaji Madini: Tunazisambaza bidhaa zetu kwenye kampuni za uchimbaji madini na kuhakikisha uendeshaji endelevu na wenye ufanisi.
Wateja wa Viwandani na Kampuni: Tunahudumia biashara na viwanda vinavyohitaji bidhaa za petroli kwa wingi kwa ajili ya shughuli zao za kila siku kupitia mifumo ya kawaida ya usambazaji na vituo vya wateja.
Wafanyabiashara Binafsi na Wauzaji Rejareja: Tunazingatia na kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara binafsi na wauzaji rejareja kote nchini.
Rejareja: Wajasiriamali na waendeshaji binafsi wanaosimamia vituo vya huduma vinavyomilikiwa na Kampuni.