Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

Tanoil Investments Limited

Masoko ya Nje ya Nchi

Biashara ya Transit katika Sekta ya Mafuta

Tanzania ni njia muhimu ya kupitishia bidhaa za petroli kuelekea nchi jirani zisizo na bandari katika Afrika Mashariki na Kati. Kwa kuzingatia nafasi ya kijiografia na uwezo wa ndani, kampuni inatumia fursa hii kutoa huduma za transit kwa kuwezesha usafirishaji wenye ufanisi wa bidhaa za petroli kutoka Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara kwenda nchi mbalimbali zikiwemo Burundi, Rwanda, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda, Zambia na Malawi.

Ulinganifu wa kimkakati umeanzishwa kupitia ushirikiano na wadau mbalimbali katika kanda ili kuhakikisha shughuli zinafanyika kwa kuzingatia mifumo ya kisheria na kikanuni, huku tukitoa bidhaa na huduma zenye ubora wa juu na za kuaminika.

Huduma Zetu za Transit Zinajumuisha:

Usimamizi wa Usafirishaji kwa Ufanisi
Tunatoa suluhisho kamili la usafirishaji kuanzia mwanzo hadi mwisho, ikiwemo huduma za bandari, usimamizi wa forodha, uchakataji wa nyaraka, na uratibu wa usafiri ili kuhakikisha usafirishaji wa bidhaa za petroli unafanyika kwa wakati ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Uhifadhi na Utoaji                                                                                                                                                                                                        Vituo vyetu vya kimkakati vya kuhifadhi vina matenki salama kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa za petroli zinazopita (transit), hivyo kuhakikisha uadilifu wa bidhaa, ubora na upatikanaji wake kwa ajili ya usafirishaji unaofuata.

Uzingatiaji wa Forodha na Kanuni
Timu yetu yenye uzoefu hushughulikia nyaraka zote za transit, taratibu za forodha, na mahitaji ya kikanuni kwa kuzingatia kanuni za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na itifaki za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), hivyo kuhakikisha usafirishaji wa mipakani unafanyika kwa urahisi.

Uhakikisho wa Ubora wa Bidhaa
Tunahakikisha udhibiti mkali wa ubora katika mchakato mzima wa transit kupitia upimaji na ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuhakikisha bidhaa zinakidhi viwango vya kimataifa na mahitaji ya nchi lengwa.

Ufuatiliaji na Utoaji wa Taarifa
Mifumo ya kisasa ya ufuatiliaji wa mizigo kwa wakati halisi huwapa wateja mwonekano wa safari ya mzigo wao kuanzia bandarini hadi kituo cha mwisho, pamoja na taarifa kamili kuhusu hali ya usafirishaji, ucheleweshaji wowote, na uthibitisho wa kuwasili.

Huduma kwa Wateja
Waratibu maalum wa huduma za transit hutoa msaada wa saa 24/7, taarifa za mara kwa mara, na utatuzi wa changamoto kwa haraka ili kuhakikisha shughuli zinaendeshwa kwa ufanisi.